Thursday, November 28, 2013

Wakulima wataka wasibanwe katika kutafuta soko

Katika siku za karibuni Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika iliwahakikishia wakulima kwa mara nyingine tena kwamba Rais Jakaya Kikwete ametoa kauli ambayo inawaruhusu wakulima kuwa huru katika kuuza mazao yao iwe kwa soko la ndani au nje.
Kauli hiyo imetolewa na msemaji wa wizara hiyo Richard Kasuga wakati akizungumza na gazeti hili.
“Kwa sasa wakulima wameruhusiwa kuuza bidhaa zao kwa namna wanavyotaka katika soko wanalotaka ili mradi wafuate sheria,” alisema Kasuga.
Wakulima hao wamesema kwamba wao ndiyo wanaochangia asilimia 95 za gharama za kilimo inakuwaje sasa wakati wakivuna Serikali ndiyo iwapangie wapi pa kuuza.
“Wakulima wanachangia asilimia 95 ya gharama za kilimo ….hakuna anayewasaidia kuanzia hatua za awali za kukodi shamba, kuliandaa, kulima , kupanda, kuondoa magugu na kuvuna. Wanafanya bila msaada lakini cha ajabu Serikali inawapangia soko, hii si sawasawa.”
 Kauli imetolewa na mmoja wa maofisa wa Chama cha Wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo Peter Lanya wakati akizungumza na Mwananchi kwenye mahojiano.
Lanya ambaye ni Makamu Mwenyekiti (kilimo) na pia Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Bidhaa nje (Tanzania Exporters Association) amesema kwamba wakulima ni vyema wakaruhusiwa kuuza bidhaa zao mahali ambapo watapata maslahi zaidi.
Alisema kwa wakulima kazi yao hiyo ndiyo inayowaingizia kipato ambacho hukitumia kwa ajili ya familia na hivyo kuwanyima nafasi ya kupata kipato kizuri si sahihi.
“Ni jambo la kustaajabisha kuwalazimisha wakulima ambao tegemeo lao la pekee la kuwapatia kipato ni kilimo kuuza bidhaa zao katika soko ambalo halina maslahi kwao. Nadhani ni vyema kuwaacha huru kutafuta masoko yenye maslahi,” alisema Lanya.
Kama wakulima hawataruhusiwa kuuza kwa namna wanayoona wao inafaa, kwa vyovyote watashindwa kuwa na kipato cha kuwasaidia kila siku na kudunduliza fedha zinazotakiwa kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo.
“Kama wasipopata fedha za kutosha kwa ajili ya matumizi ya msingi ya kwao wenyewe kama matibabu hawatakuwa na uwezo wa kufanya shughuli za kilimo kwa msimu unaofuata na hivyo kuongeza kasi ya umaskini,” alisema Lanya.
Hata hivyo alionya wageni wanaofika nchini na kununua mazao yakiwa bado shambani kabla ya msimu wa mavuno.

Njia mpya ya Reli Afrika Mashariki


 
Kenya imezindua rasmi ujenzi wa njia ya Reli itakayounganisha kanda ya Afrika Mashariki na eneo la maziwa makuu ujenzi utakaofadhiliwa na serikali ya China.
Reli hiyo itaunganisha Kenya na Sudan Kusini, DR Congo na Burundi.
Sehemu ya kwanza ya njia hiyo ya reli , itaunganisha bandari ya Mombasa na Mji mkuu Nairobi na kupunguza muda wa safari kati ya miji hiyo kutoka masaa 15 hadi masaa manne tu.
Huu bila shaka ndio utakuwa mradi mkubwa Zaidi kuwahi kujengwa tangu nchi hiyo kujipatia uhuru miaka 50 iliyopita.
Mradi huo utagharimu dola bilioni 5.2 kiasi kikubwa cha pesa hizo kikitolewa na Uchina.
Baadhi ya wakenya wanalalamika kuwa tenda hiyo imetolewa kwa kampuni ya kichina kwa njia isiyofaa.
Rais Uhuru Kenyatta katika hafla ya uzinduzi huo amesema kuwa mradi huu ndio utakuwa kumbukumbu kubwa ya utawala wake Kenya.
Mkataba wa ujenzi wa njia hiyo ya reli, ulifikiwa kati ya Rais Kenyatta na mwenzake wa China Xi Jinping mnamo mwezi Agosti mjini Beijing.
Pia kuna matumaini kuwa njia hiyo ya reli itapunguza msongamano mjini Mombasa moja ya bandari yenye shughuli chungu nzima barani Afrika.
Njia ya reli iliyoko sasa, ni ile iliyojengwa enzi za ukoloni.
Baada ya kukamilika kwa sehemu ya kwanza ya reli hiyo mjini Nairobi, mwaka 2017, itaendelezwa hadi Magharibi mwa DRC hususan mjini Kisangani, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
"Tunachokifanya hapa leo, kitaleta mageuzi makubwa sio nchini Kenya tu bali katika kanda nzima ya Afrika Mashariki,’’ alisema Rais Kenyatta akitaja mradi huo kama jambo la kihistoria.
Aliongeza kusema kuwa mradi huu ni moja ya miradi mikubwa katika maono yake ya maendeleo itimiapo mwaka 2030 kuboresha hali ya miundo msingi nchini humo.

Wednesday, November 27, 2013

Serikali yatangaza nafasi za kazi 2,748

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania  wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 2,748 kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa Ofisi za Umma.
Daudi alitaja nafasi za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa Uvuvi daraja la ii, Mvuvi msaidizi daraja la ii, Afisa Mifugo msaidizi daraja la ii, Afisa mifugo daraja la ii, Mteknolijia wa samaki daraja la ii, Daktari wa mifugo daraja la ii,Afisa utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari utafiti Mifugo daraja la ii, Fundi sanifu Maabara Mifugo daraja la ii, Mkufunzi Mifugo daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo msaidizi na Daktari Mifugo.
Kada nyingine ni Mkufunzi daraja la ii, Mtekinolojia wa Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti daraja ii, nafasi 2, Dereva wa vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa kilimo daraja la ii, Afisa kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi kilimo daraja la ii, Fundi sanifu daraja la ii, Afisa utafiti kilimo daraja la ii, Mkufunzi wa kilimo msaidizi, Afisa kilimo msaidizi daraja la iii,Dereva daraja la ii, mlinzi, Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha mkuu iii  na Afisa vipimo.

Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira nafasi hizo za kazi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpanda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nkasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sumbawanga na Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni.

Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chato, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misenyi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ngara, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukoba, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilindi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Korogwe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Pangani, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Korogwe na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muheza.

Nafasi hizo pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulyankulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uyui, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nzega, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Nzega, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Manispaa ya Tabora, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ikungi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iramba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Manyoni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Singida, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Itilima na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ushetu.

Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Msalala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kishapu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Meatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bariadi, Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyasa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Namtumbo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Manispaa ya Songea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyang`wale, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ukerewe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Geita na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Magu.

Nafasi hizo za kazi pia ni kwa aajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Newala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Masasi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Gairo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mvomero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilombero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Morogoro, Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Tunduma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Momba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbarali, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ileje, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chunya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbozi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbeya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rorya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Serengeti, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bunda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tarime, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Butiama, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ruangwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nachingwea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Lindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mwanga na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Hai.

Katika nafasi hizo waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rombo, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Moshi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uviza,  Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Monduli, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Babati, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Hanang, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Simanjiro, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iringa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makete, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chamwino, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kongwa na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bahi, 

Waajiri wengine katika nafasi hizo za kazi ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilolo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ludewa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Wanging`ombe, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya  Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kasulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kakonko, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu Tawala Mkoa Pwani, Katibu Tawala Mkoa Dodoma, Katibu Tawala Mkoa Iringa, Katibu Tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu Tawala Mkoa Mtwara, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Katibu Tawala Mkoa Ruvuma, Katibu Tawala Mkoa Tabora, Katibu Tawala Mkoa Kagera, Katibu Tawala Mkoa Dar es salaam, Katibu Tawala Mkoa Rukwa, Katibu Tawala Mkoa Katavi, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa  Simiyu na Katibu Tawala Mkoa Geita.

Daudi amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 10 Desemba, 2013. Aidha amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kutambua kwamba Kila mwombaji kazi atapangwa katika kituo chochote cha kazi bila kujali eneo au mahali alipoomba kutokana na mahitaji ya mwajiri pamoja na idadi ya waombaji katika eneo husika.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 27 Novemba, 2013.